Serikali imesema imeleta mabadiliko katika sekta ya elimu iliyokuwa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mpito wa elimu ya umilisi, upungufu wa walimu, na changamoto za ufadhili katika vyuo vikuu, pamoja na changamoto za miundo mbinu. Rais William Ruto wakati wa taarifa yake kwa taifa kwenye kikao cha pamoja cha bunge, alibainisha kuwa kupitia mfumo wa ufadhili unaotilia maanani mahitaji ya wanafunzi, zaidi ya wanafunzi nusu milioni wamenufaika na ufadhili wa elimu na mikopo ya elimu ya vyuo vikuu. Rais alisema kuwa uajiri wa walimu, ujenzi wa madarasa , maabara na ongezeko la wanafunzi katika taasisi za mafunzo ya kiufundi ni muhimu katika kurejesha heshima na fursa katika sekta ya elimu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive