Kuna haja ya uwekezaji zaidi katika dawa za kiasili, ili kupanua fursa za huduma za afya humu nchini. Mkurugenzi wa kampuni ya Harriet Botanicals, Harriet Chebet, alisema uwekezaji unaoambatana na usaidizi wa sera katika suluhu za kitamaduni utasaidia pakubwa kwa pamoja na huduma za afya za kisasa, na kupanua fursa za matibabu kwa wakenya. Alikuwa akizungumza wakati wa tuzo za mwaka huu za wakurugenzi bora 100 jijini Nairobi ambako kampuni yake iliibuka ya pili katika kitengo cha utengenezaji bidhaa na uvumbuzi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive