Serikali imekariri haja ya kuwekeza katika kilimo, marekebisho ya ushuru, ubunifu na teknolojia ili kuzalisha rasilmali zake na kukoma kutegemea zaidi usaidizi wa kigeni. Akizungumza jijini Nairobi wakati wa kongamano la kwanza na uzinduzi wa mpango wa miaka kumi wa kongamano kuhusu utafiti wa kiuchumi barani Afrika katibu wa mipango ya kiuchumi Dr Boniface Makokha, pia alitoa wito wa kujumuisha utafiti katika mipango y ustawi. Kongamano hilo linanuiwa kuimarisha uwezo wa utafiti huru na kabambe kuhusu usimamizi wa kiuchumi barani Afrika.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive