Wakazi wa vijiji vya Kabuteti na Karangi eneo bunge la Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu, wamelalamikia hali duni ya barabara muhimu ambazo hazipitiki huku zikitatiza usafirishaji na shughuli muhimu za kiuchumi za kila siku. Hali ya muundombinu katika maeneo hayo imekuwa mbaya zaidi baada ya daraja kuu linalounganisha milima miwili kuporomoka miezi kadhaa iliyopita. Licha ya wakaazi kuripoti tukio hilo, daraja jipya bado halijajengwa, jambo linalolazimisha jamii kutegemea daraja la muda lililotengenezwa kwa mbao na vyuma.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive