Kenya na nchi nyingine 18 za Afrika Mashariki, Kusini na Kaskazini zimeongeza juhudi za kuanzisha kampuni ya pamoja ya usafiri wa meli kama sehemu ya mikakati mipana ya kulinda uchumi wao dhidi ya misukosuko ya kimataifa, changamoto za usambazaji bidhaa na ongezeko la bei ya bidhaa. Wawakilishi wa nchi hizi, wanaokutana jijini wanatathmini ripoti za awali za upekuzi yakinifu kuhusu kuanzishwa kwa kampuni ya usafiri wa meli pamoja na itifaki ya kikanda ya mizigo ya baharini inayolenga kuimarisha udhibiti wa Afrika juu ya biashara ya baharini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive