Gavana wa Kaunti ya Mandera, Mohamed Adan Khalif, ameonya kwamba ukame unaoikumba kaunti hiyo umefikia kiwango cha janga. Kulingana na Gavana huyo, wakazi sasa wanategemea visima visvyo na maji, huku mabwawa ya maji yakiwa yamekauka, na kuwaacha maelfu ya familia zikiwa na hitaji kubwa la msaada. Gavana huyo ametoa wito wa haraka kwa Serikali ya Kitaifa na mashirika ya kibinadamu kuingilia kati kabla hali hiyo haijakithiri.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive