Shirika la utangazaji nchini KBC, limepata ushindi mahakamani kwenye kesi ya muda mrefu ya mzozo wa ardhi. Hii inajiri baada ya mahakama ya kusikiza kesi za ardhi na kimazingira katika kaunti ya Machakos kuamua kwamba shirika la KBC, ndio mmliki wa shamba la takriban hekta 500 katika eneo la Komarock, kaunti ya Machakos ambako kuna kituo cha mitambo ya upeperushaji matangazo. Kwenye uamuzi uliotolewa leo , mahakama hiyo ilisema ardhi hiyo ilio kwenye barabara ya Kangundo , ilitwaliwa na serikali kwa minajili ya utangazaji na kwamba chama cha umiliki ardhi cha Komarock kilipewa fidia .
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive