Miito kwa wanawake kuchukua hatua katika uongozi wa taifa hili ilitolewa wakati wa sherehe ya kumkumbuka Phoebe Muga Asiyo. Sherehe hiyo ya ukumbusho iliyoandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi iliwavutia wanawake viongozi, marafiki na jamaa wakimkumbuka Asiyo kama kiongozi mashuhuri aliyejitolea kupigania haki za wasiojiweza katika jamii. Asiyo aliyefariki mwezi Julai mwaka 2025, anakumbukwa kwa mchango wake katika utumishi wa umma akiwa mwanamke wa kwanza nchini kuwa msimamizi mwandamizi wa magereza na vilevile mbunge wa Karachuonyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive