Serikali imetangaza mipango ya kuongeza mgao wa hazina ya kitaifa ya utafiti kama mbinu ya kuimarisha utoaji uwezo kupitia ukuzaji wa ujuzi, kuongeza maarifa na kupiga jeki ubunifu na uvumbuzi. Rais William Ruto amesema hatua hiyo itaongeza mgao wa bajeti wa utafiti wa taifa hili hadi shilingi trilioni moja katika kipindi cha mwongo mmoja ujao, na kuviwezesha vyuo vikuu kuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi na ustawi wa kiteknolojia. Rais aliyasema hayo wakati wa sherehe ya tatu ya mahafali ya chuo kikuu cha kitaifa cha Ulinzi nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive