- 9,109 viewsDuration: 4:52RaisWilliam Ruto ametangaza vinono kwa maafisa wa utawala ikiwemo malipo kwa zaidi ya wazee laki moja wa vijijini, kupandishwa vyeo kwa machifu na pia makonstebo wa polisi walio na umri wa miaka 50 na zaidi. Rais aliyasema hayo alipopokea ripoti ya mpango wa Jukwaa La usalama kutoka kwa wizara ya usalama. Ripoti hiyo ilipendekeza mpango wenye vipengee 21 wa kuimarisha usalama yakiwemo maslahi na usaidizi wa maafisa, marekebisho ya sera ya kisheria na kitaasisi, kuimarisha usalama mtandaoni, kugatuliwa kwa huduma za uhamiaji, kudhibitiwa na kupewa uwezo wa kwa sekta ya Boda Boda. Mwanahabari wetu Giverson Maina anatuarifu zaidi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive