USAJILI WA MAKURUTU WA POLISI
Shughuli ya siku moja ya usajili wa makurutu wa polisi ilifanyika katika vituo vyote 427 kote nchini, huku idadi wa waliojitokeza katika baadhi ya vituo hivyo ikiwa ya chini mno. Huduma ya taifa ya Polisi iliyotathmini shughuli hiyo ilisema kuwa ilikuwa huru na ya haki bila visa vya ufisadi kunakiliwa. Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, ambaye alikuwa katika kaunti ya Narok kushuhudia shughuli hiyo, alisema kuwa ilitekelezwa kwa ufanisi na kwamba huduma hiyo inanuia kusajili makurutu watakaojiunga na kizazi kipya cha maafisa wenye mtazamo wa mageuzi watakaosaidia kujenga upya imani ya umma kwa polisi, pamoja na kuandaa mazingira thabiti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive