Katibu wa usalama wa taifa dakta Raymond Omollo ameonya kwamba serikali inakabiliwa na ongezeko la tishio la uhalifu wa kimtandao, hali ambayo imeweka Kenya kuwa miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yanapoteza zaidi ya dola bilioni-4 kila mwaka kutokana na uhalifu wa kimtandao. Akiongea katika kaunti ya Nairobi leo wakati wa kufunguliwa kwa kikao cha tatu cha Afrika kuhusu uhalifu wa kimtandao na kielektroniki, dakta Omollo alitoa wito wa ushirikiano dhabiti wa kimataifa na ushirikishaji kamili wa vijana katika kudumisha usalama mitandaoni.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive