Mwenyekiti wa halmashauri ya usimamizi wa Viwanja vya Ndege , Caleb Kositany, amezitaka taasisi za elimu ya juu humu nchini kuanzisha kozi za mafunzo ya urubani kwenye ngazi ya shahada ili kukidhi hitaji linaloongezeka katika sekta hiyo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Shule ya Urubani humu nchini na Chuo Kikuu cha Baraton East Africa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Kositany alisema nchi hii inakabiliwa na uhaba mkubwa wa marubani na inalazimika kuajiri raia wa kigeni kufanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Wakenya.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive