Wataalamu kutoka shirika la IGAD wametoa wito kwa washirika wa kimaendeleo kuchunguza upya kuhusu uamuzi wao wa kusitisha misaada ya kifedha, ambayo ilikuwa ukikidhi mahitaji ya kibinadamu. Wataalamu hao wanasema hatua hiyo haijasababisha kupunguzwa kwa bajeti katika sekta muhimu pekee, bali pia imesababisha vifo vya watu. Wataalamu hao waliokuwa wakizungumza wakati wa mkutano wa utathmini ulioandaliwa jijini Nairobi kuhusu azimio la Nairobi, waliwahimiza wanachama wake kuwekeza katika mikakati ya muda mrefu ambayo itakayodumisha maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive