- 176,446 viewsDuration: 1:13Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema miongoni mwa mambo yanayowasikitisha Watanzania kwa sasa ni kutokiri ukweli kwamba waliouawa wameuawa na nani, huku akihoji kwamba ilikuwaje vyombo vya usalama havikufanikiwa kuzuia mauaji yaliyojitokeza. Akizungumza na Jambo TV, Desemba 1, 2025, Padre Kitima amesema kwamba tafakari ya Maaskofu imebainisha wazi kwamba waliohusika na mauaji wanapaswa kuwajibika. “Tunachosikitika mpaka sasa na wanachosikitika Watanzania, wanachoumia Watanzania mpaka sasa, kinyume na mila na desturi za makabila yote ya Tanzania mpaka sasa ni kutokukiri ukweli kwamba, waliouawa wameuawa na nani? na kama aliyeua hatambuliki, ilikuwaje vyombo vinavyozuia mauaji visifanikiwe kuzuia mauaji?” ameeleza Padre Kitima kwa kuhoji. Akirejelea katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 14, amesema kila raia wa nchi ya Tanzania ana haki ya uhai wake na ana haki ya kupata hifadhi ya uhai wake. Amesisitiza kwamba ili kusonga mbele ni lazima mamlaka zikiri kilichofanyika. - - #Bbcswahili #maandamano #dini #siasa #tec #kanisakatoliki #uchaguzimkuu2025