Athari za kimbunga Hidaya zaanza kudhihirika Pwani

  • | K24 Video
    12,369 views

    Idara ya utabiri wa hali ya hewa humu nchini imetangaza kuwa athari za kimbunga Hidaya zimeanza kudhihirika katika Pwani ya Kenya, na kufikia kesho, kutakuwa na mvua kubwa mno katika kaunti za eneo hilo. Kufuatia hilo, serikali ya kaunti ya Kilifi imepiga marufuku shughuli za uvuvi bahari hindi, hadi pale kimbunga hidaya kitakapomalizika.