Baadhi ya shule Kisumu zatumika kama makao ya muda

  • | Citizen TV
    712 views

    Huku mafuriko yakizidi kuhangaisha, shule zikisombwa na maji na waathiriwa wa mafuriko wakitafuta hifadhi shuleni, waziri wa elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu ufunguzi wa shule wiki ijayo. haya ni huku baadhi ya wanafunzi na wazazi wao wakiachwa bila makao, barabara zikifurika na madaraja kusombwa na maji, jambo ambalo linakisiwa kuhatarisha usafiri wa wanafunzi, haswa wa shule za kutwa. kwa sasa machogu anahudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka mia moja ya shule za kiufundi katika taasisi ya kiufundi ya Kabete.