Hazina ya kusaidia dharura imezinduliwa hapa nchini

  • | Citizen TV
    4,042 views

    Serikali sasa inaomba msaada kuwasaidia waathiriwa wa janga la mafuriko huku ikizindua hazina ya kushughulikia janga hili. Naibu Rais Rigathi Gachagua anasema kuwa hazina hii itasaidia serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushughulikia kwa dharura mahitaji ya zaidi ya watu laki tatu walioathirika na mafuriko. Haya yakijiri huku Rais William Ruto akizuru eneo la Mathare hapa Nairobi, ambako amewaahidi waathiriwa msaada na makao mapya kwenye mpango wa nyumba za nafuu za serikali.