Rais Ruto aagiza wizara ya elimu kuahirisha ufunguzi wa shule kwa muda usiojulika

  • | K24 Video
    177 views

    Rais William Ruto ameagiza wizara ya elimu kuahirisha ufunguzi wa shule kwa muda usiojulikana kufuatia athari za mvua kubwa inayoendelea katika maeneo tofauti nchini. Kulingana na serikali shule 1,967 zimeharibiwa na mafuriko na haziwezi kutumiwa na wanafunzi. Haya yanajiri wakati wakazi wa pwani wakionywa kuhusu mvua kubwa itakayoanza wakati wowote kutokana na kimbunga hidaya.