Serikali yaruhusiwa kutumia pesa zaidi ili kukabiliana na athari za mafuriko

  • | K24 Video
    84 views

    Serikali sasa imeruhusiwa kutumia pesa zaidi ili kukabiliana na athari za mafuriko yanayoshuhudiwa kote nchini. Kamati ya bunge kuhusu bajeti sasa inasema itaidhinisha pesa zozote zinazotengewa kusaidia waathiriwa wa mafuriko huku idadi ya walioangamia kutokana na mafuriko ikifika watu 60, na wakaazi katika eneo la Uthiru 87 ulio mpaka wa kaunti za Nairobi na Kiambu wamesalia na hofu baada ya sehemu hiyo kushuhudia maparomoko ya ardhi. Haaya yanajiri huku watu watatu wakisombwa na maji kaunti ya Nandi idadi sawia na kaunti ya Turkana