Wakazi wa vijiji vyaGoda na Bulesa katika wadi ya Chari, kaunti ya Isiolo County, wana sababu ya kutabasamu kufuatia kukamilika kwa mradi wa maji ambao utakomesha dhiki ya uhaba wa maji ya miongo mingi na safari ndefu ya kwenda kuteka maji kwenye Mto Ewaso Nyiro.
Mradi huo unaotekelezwa na serikali ya kaunti kwa ushirikiano na shirika la Kenya Rapid Plus chini ya Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki utajumuisha kisima kinachotumia kawi ya miale ya jua, mabomba ya urefu wa kilomita nne na tangi la kuhifadhi maji la lita 50,000. Wakazi wanasema mradi huo utainua viwango vya usafi, kuboresha upatikanaji chakula na kuwalinda wanawake kutokana na tisho la uvamizi wa wanyama pori wanapokwenda mtoni kuteka maji,
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive