Mahakama kuu imesitisha utekelezaji wa baadhi ya vipengee vya sheria ya matumizi mabaya ya tarakilishi na uhalifu mtandaoni, ya mwaka 2024 iliyotiwa saiani na rais William Ruto siku ya Jumatano tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2025. Jaji Lawrence Mugambi wa mahakama kuu alihimiza pande husika kuwasilisha majibu yao katika muda wa wiki mbili zijazo huku kesi hiyo ikitarajiwa kusikilizwa tarehe 5 mwezi Novemba mwaka 2025. Katika kesi hiyo, walalamishi wamesema sheria hiyo inakiuka haki za kimsingi zilizoratibishwa kwenye katiba wakidai itakandamiza uhuru wa kujieleza.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive