Skip to main content
Skip to main content

Serikali yatoa msaada kwa familia za waathiriwa Mombasa

  • | KBC Video
    283 views
    Duration: 1:55
    Familia tatu ambazo zilipoteza wana wao katika ajali ya mashua wakati wa Tamasha la Bahari la Afrika Mashariki mjini Mombasa wiki mbili zilizopita zimepata faraja, huku shinikizo za hatua kabambe za kuimarisha usalama katika michezo ya majini eneo la pwani zikiendelea kutolewa. Akizungumza wakati alipotembelea familia hizo zinazoomboleza naibu rais, Profesa Kithure Kindiki alitoamchango wa shilingi milioni tatu kusaidia familia hizo katika mipango ya mazishi iliyositishwa kutokana na vikwazo vya kifedha. Ajali hiyo ilitokea wakati boti iliyokuwa na washiriki 22 ilipopinduka na kuzama. Juhudi za dharura zilifamikisha kuopolewa kwa watu 19, lakini watatu wakazama. Mili yao ilipatikana siku tatu baadaye kupitia operesheni iliyohusisha mashirika mbalimbali chini ya uongozi wa Jeshi la wanamaji la Kenya. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive