Skip to main content
Skip to main content

Ogamba awataka wahadhiri wa vyuo vikuu kurejea kazini

  • | KBC Video
    68 views
    Duration: 2:31
    Serikali imewataka wahadhiri wanaogoma warejee kazini.Akiongea huko Mombasa, waziri wa elimu Julius Ogamba alionya kwamba mahakama tayari imeamua mgomo huo ulioanza wiki iliyopita, kuwa haramu. Waziri huyo alisema utoaji wa shilingi bilioni 2.73 ni ishara ya kujitolea kwa serikali kufanya mazungumzo ili kusuluhisha masuala mengine yaliyopo. Wakati uo huo, chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu hapa nchini UASU kimesema wanachama wake hawatarejea kazini hadi malimbikizi yote kwenye mkataba wa maelewano wa mwaka 2017-2021 yatakapolipwa kikamilifu, na mazungumzo na kutiwa saini kwa mkataba wa mwaka 2025-2029 vitekelezwe, kikisema hatua hiyo ilitarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka 2025. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive