Wizara ya ustawishaji wa vyama vya ushirika na biashara ndogo ndogo, inanuia kutumia bajeti ya ziada ya mwezi Novemba, kushinikiza utoaji wa shilingi milioni 204 za malipo ya kuhudumu ya wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya maziwa ya KCC. Waziri wa vyama vya ushirika Wycliffe Oparanya aliambia kamati ya leba katika bunge la seneti kuwa mwanasheria mkuu alikuwa ametoa ushauri kwamba kamati ya pamoja ya wizara mbalimbali ibuniwe, kuongoza mpango wa utoaji malipo kwa wafanyakazi hao wa zamani ambayo yamekwama tangu mwaka wa 1998.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive