- 59 viewsDuration: 2:38Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen ameihakikishia nchi hii kwamba mpaka baina ya Kenya na Somalia ni salama na kwamba ripoti kuhusu mashambulizi kutoka Somalia katika kaunti ya Mandera si ya kweli. Waziri aliyeyasema hayo wakati wa kikao cha Jukwaa La Usalama pia alisema kuwa machifu katika kaunti ya Mandera watapewa bunduki za kujikinga. Hii ni baada ya machifu wanne wa eneo hilo kutekwa nyara mwezi Februari mwaka huu na kuachiliwa miezi miwili baadaye. Mwanahabari wetu Giverson Maina yuko katika kaunti ya Mandera na ametuandalia taarifa ifuatayo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive