Wakazi wa miji ya Sagana, Kagio na Wang’uru wameunga mkono pendekezo la Serikali ya Kaunti ya Kirinyaga la kuunda manispaa mbili mpya. Hatua hiyo inalenga kuimarisha mipango ya miji, kuboresha miundombinu, na kufungua fursa za ufadhili kutoka kwa Serikali Kuu pamoja na washirika wa maendeleo.Kulingana na pendekezo hilo, miji ya Sagana na Kagio itaunganishwa kuwa manispaa moja, huku Wang’uru ikibaki kama manispaa huru. Waziri wa Ardhi, Makazi na Maendeleo ya Miji, katika kaunti hiyo Mchungaji Samuel Kajobe, alieleza kuwa mpango huo unapata msukumo kutokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu, kuimarika kwa shughuli za biashara, na haja ya usimamizi bora wa miji ili kuendeleza uchumi unaokua kwa kasi katika miji hiyo mitatu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive