Maafisa wa afya katika Kaunti ya Nandi wameanzisha kampeni ya uhamasisho kuhusu saratani katika vituo vyote vya afya katika kaunti hiyo, kwa lengo la kuhimiza matibabu ya mapema na kuzuia ugonjwa huo kuenea mwilini.Afisa mkuu wa matibabu wa Kaunti ya Nandi anayesimamia matibabu ya saratani, Patrick Kenei, amethibitishakuwa utafiti umeanzishwa ili kubainisha ongezeko la visa vya saratani katika kaunti hiyo.Akizungumza katika kijiji cha Kaptich, eneo bunge la Mosop, Kenei alisema kuwa Hospitali ya matibabu maalum ya Kapsabet inapokea wagonjwa zaidi ya watano kila mwezi wanaougua aina mbalimbali za saratani.
Amewataka wakazi kujisajili na Hamashauri ya Afya ya Jamii (SHA), kula lishe bora, na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kudhibiti magonjwa hayo. Wakati huohuo, waendeshji baiskeli katika mji wa Kapsabet, Kaunti ya Nandi, walishiriki katika shindano la kuendesha baiskeli kwa umbali wa kilomita 70 kutoka Kapsabet hadi kituo cha Ndurio, eneo bunge la Aldai, na kurejea — kama sehemu ya uhamasisho kuhusu saratani ya titi katika jamii na umuhimu wa uchunguzi wa mara kwa mara wa saratani.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive