Serikali itawatunuku tuzo za rais machifu watano waliotekwa nyara huko Mandera wakiwa kazini. Akiongea huko Mandera wakati wa mazungumzo ya ushirikishaji umma kwenye masuala ya usalama katika kaunti, almaarufu Jukwaa la usalama, Kipchumba Murkomen aliwakosoa wakoaji wa serikali kwa kudai awali kwamba serikali ilishauriana na magaidi wa Al-Shabaab wakati machifu watano walitekwa nyara huko Mandera mwezi Februari, na kuachiliwa huru mwezi Aprili mwaka huu. Murkomen alisema serikali inatambua kujitolea na uzalendo wa maafisa hao wa utawala waliohatarisha maisha yao ili kulilinda taifa hili. Giverson Maina anaarifu Zaidi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive