Mgomo wa wafanyakazi wa shirika la Posta umeingia siku ya tatu, ukidumaza huduma za utumaji barua na usafirishaji vifurushi katika vituo vingi vya Huduma kote nchini. Wafanyakazi hao wanadai malipo ya mishahara yao ya miezi sita na kuwasilishwa kwa matozo yao kwa taasisi husika. Mamia ya wafanyakazi hao waliandamana jijini Nairobi kutoka eneo la City Square hadi makao makuu ya shirika la Posta, wakiimba na kubeba mabango wakitaka kulipwa mishahara yao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive