- 93 viewsDuration: 1:44Wizara ya afya imeweka juhudi kuhakikisha huduma za afya ya meno zinawafikia Wakenya wote kwa urahisi na kwa gharama wanaypoweza kumudu. Haya yanawadia huku kikiwa na hofu kwamba Wakenya wengi wanashindwa kupata huduma hizo kutokana na gharama ya juu huku zikiwa nadra katika vituo vya afya vya umma.Mkurugenzi wa afya Dkt. Patrick Amoth amesema hali hii inakuwa mbya zaidi kwa vile huduma za afya ya meno hazijajumuishwa kwenye Halmashauri ya Afya ya Jamii. Akihutubia kongamano la wataalamu wa meno katika kaunti ya Kwale, Dkt Amoth alisisitiza haja ya kupatia afya ya mdomo kipaumbele na kuijumuisha kwenye mpango wa afya kwa wote. Madaktari wa meno waliohudhuria kongamano hilo walizitaka serikali za kaunti kuwaajiri wataalamu zaidi kushughulikia uhaba uliopo huku wakiwataka Wakenya kuchunguzwa mara kwa mara kuhusu afya yao ya mdomo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive