- 5,625 viewsDuration: 2:43Shule zote za bweni sasa zitatoza karo sawa baada ya serikali kuondoa kabisa mfumo wa kuainisha shule za upili za umma. Mwongozo wa mpito wa sekondari ya juu umeelekeza shule zote za umma za bweni kutoza karo ya shilingi 53,000 kwa mwaka. Mwongozo huo pia umetoa mwelekeo kuhusu idadi ya vipindi kwa kila somo katika shule za sekondari ya juu kuanzia mwezi januari mwaka ujao.