Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imeagizwa kuchunguza madai ya wizi wa mali ya umma katika kaunti ya Trans Nzoia. Hii ni baada ya mapato yanayokusanywa na kaunti hiyo, kupungua kwa shilingi milioni 20 katika kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2023/2024. Akiwa mbele ya kamati ya uhasibu wa pesa za umma katika bunge la seneti kujibu maswali yaliyoibuliwa na mkaguzi mkuu wa matumizi ya pesa za serikali, Gavana George Natembeya alitakiwa kuelezea ni kwa nini kaunti hiyo imekusanya shilingi milioni 261 pekee dhidi ya lengo la shilingi bilioni 2.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive