Wagombea urais David Maraga na Reuben Kigame wamewataka Wakenya kuwakataa wanasiasa wala rushwa na badala yake kuwakumbatia viongozi wenye maono kwa taifa hili. Wakiwahuubia waombolezaji kwenye hafla ya mazishi huko Makueni, Maraga alisema taifa lina uwezo mkubwa wa maendeleo, lakini Wakenya lazima wachague viongozi sahihi ili kufanikisha mageuzi hayo. Wakati huohuo, Chama cha Jubilee, tawi la Kisii limetangaza kumuunga mkono aliyekuwa Waziri wa Usalama wa taifa Dkt. Fred Matiang’i katika azma yake ya kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News