Wazazi wa shule ya upili ya wavulana ya Gatunguru huko Gatundu kaskazini, kaunti ya Kiambu, wanalalamikia agizo la shule hiyo linalomtaka kila mwanafunzi kulipa shilingi elfu-25 ili kujenga upya mabweni matatu ya shule hiyo yaliyoteketea majuma mawili yaliyopita. Kisa hicho kilichosababisha kuteketea kwa mabweni hayo ingawa hakuna majeruhi walioripotiwa, kimewalazimu wanafunzi kusalia nyumbani kwa wiki mbili, hali ambayo imetatiza masomo. Kwengineko wazazi wa shule ya Hillside Endarasha Academy iliyoshuhudia kisa cha moto mwaka 2024, wamewasilisha kesi mahakamani, kutafuta haki kwa watoto wao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive