Walimu-10 washtakiwa Homa Bay kwa kupanga njama ya udanganyifu wa mtihani

  • | KBC Video
    23 views

    Watahiniwa wawili wanazuiliwa na polisi huko Ruiru, kaunti ya Kiambu baada ya kudaiwa kuhusika katika udanganyifu kwenye mtihani wa kitaifa unaoendelea wa kidato cha nne, KCSE. Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa idara ya upelelezi, eneo la Ruiru Jeremiah Ndumbai, alisema watahiniwa hao ambao ni wanafunzi katika shule ya upili ya Membely walipatikana na simu katika kituo cha mtihani. Hayo yakijiri walimu kumi wa shule ya sekondari ya Pala Masogo wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja na mahakama ya Homa Bay baada ya kukanusha mashtaka ya kupanga njama ya udanganyifu kwenye mtihani huo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive