Serikali yafutilia mbali mpango wa kugharamia elimu ya bure ya vyuo vikuu

  • | K24 Video
    51 views

    Serikali imefutilia mbali mpango wa kugharamia elimu ya bure ya vyuo vikuu, ikisema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 900 zinazohitajika hazitapatikana. Haya yanajiri baada ya wasiwasi kuibuka kutoka kwa wabunge kuhusu matumizi mabaya ya fedha yaliyotengewa wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali katika vyuo vikuu vya kibinafsi. Kulingana na idara ya huduma za usajili wa wanafunzi katika vyuo vikuu na vile vya anuwai, hakuna namna ya kuwafuatilia wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali, na hivyo basi hakuna uhakika iwapo fedha hizo zinatumika ipasavyo. Wakati huo huo, bodi ya hazina ya vyuo vikuu imesitisha utoaji wa fedha kwa muhula wa pili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ikisubiri mwelekeo kutoka kwa mahakamani.