Magavana wataka mgao wa kaunti uongezwe hadi Ksh.400b

  • | Citizen TV
    554 views

    Mgawanyiko umezidi kuibuka kwenye kikao cha kamati ya upatanisho kuhusu ugavi wa rasilmali kati ya serikali kuu na serikali za kaunti huku mwenyekiti wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu bajeti Ndindi Nyoro akisisitiza kuwa kuna upungufu wa shilingi bilioni 788 kwenye bajeti ya mwaka huu wa kifedha. Maseneta wamesisitiza kuwa hawatakubali kupunguzwa kwa mgao wa kaunti, ikiarifiwa kuwa kaunti zinaidai serikali kuu zaidi ya shilingi bilioni 30.