Mshukiwa wa mauji ya wanawake ni raia wa Ethiopia

  • | Citizen TV
    172 views

    Mshukiwa wa mauaji ya mwanamke mmoja na mabinti wawili wa familia moja katika mtaa wa Eastleigh ni raia wa Ethiopia ambaye ana kitambulisho cha Kenya. Akitoa taarifa ya mauaji na utekajinyara nchini katika kamati ya bunge kuhusu usalama, Inspekta jenerali wa polisi, Douglas Kanja amesema kuwa mshukiwa huyo alikuwa na wake watatu nchini Ethiopia na alimuua mmoja pamoja na wanawe watatu. Mshukiwa huyo pia anahusishwa na mwili uliopatikana umekakatatwa katika makaburi ya Lang'ata.