Waziri Aden Duale apiga marufuku shughuli za kilimo katika misitu ya asili kote nchini

  • | K24 Video
    2 views

    Waziri wa mazingira Aden Duale amepiga marufuku shughuli za kilimo katika misitu ya asili kote nchini, akisisitiza kuwa kilimo kimeharibu pakubwa shughuli za uhifadhi misitu. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa zaidi ya shilingi milioni 600 wa kufufua uhifadhi wa mlima Elgon, eneo la keberewa, waziri huyo ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha na shughuli za kilimo katika msitu wa mlima Elgon..Duale pia ametangaza kuwa serikali imetenga tarehe 7 novemba kila mwaka kuwa siku maalum ya kuhamasisha wakazi mlima elgon kuhusu umuhimu wa kukuza na kulinda miti.