Rais asema serikali itaboresha mandhari jijini Nairobi

  • | KBC Video
    155 views

    Rais William Ruto amesema kuwa serikali imejitolea kuboresha mandhari ya Jiji la Nairobi kwa kuondoa taka na kunadhifisha Mito ya Nairobi, Mathare na Ngong. Rais alisema kuwa likiwa jiji kuu la taifa hili, Nairobi ni kitovu muhimu katika kanda ya Afrika Mashariki na hadhi yake ni sharti irejeshwe kufikia viwango vilivyoachwa na aliyekuwa waziri wa mazingira, Marehemu John Michuki. Alisema haya alipokutana na Gavana wa Nairobi, wabunge wa kaunti hii na tume ya mito ya Nairobi katika Ikulu ya Nairobi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive