Mauaji Kware I Serikali yashutumiwa kwa kujikokota kukamilisha uchunguzi

  • | KBC Video
    31 views

    Watetezi wa haki za binadamu wanaikashifu serikali kwa kile wanachosema kuwa kuchelewesha kimakusudi uchunguzi kuhusu mauaji ya watu kadhaa katika jalala la Kware lililoko mtaa wa Mukuru kwa Njenga jijini Nairobi. Wakiongozwa na shirika la Haki Africa, mashirika hayo yalitaja kukosa kukamatwa kwa mshukiwa mkuu Collins Jumaisi aliyetoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi katika mazingira yasiyoeleweka. John Kahiro ana maelezo zaidi kuhusu shinikizo za kuanzishwa tena kwa shughuli ya kutafuta miili zaidi inayoaminika kuwa bado imenaswa katika timbo hilo huku familia za waathiriwa zikililia haki.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News