- 614 viewsMamia ya wanafamilia waliokata tamaa kwa ajili ya ndugu zao wachimba madini haramu waliokwama kwenye mgodi Afrika Kusini wamemiminika nje ya mgodi huo wakisubiri kwa matumaini kuwa wapendwa wao watatoka chini ya ardhi. Wachimbaji wako katika mvutano na polisi ambao wamezuia kupelekewa chakula na maji, na wanajaribu kuwalazimisha kutoka ili wakamatwe kwa sababu ya kuingia kinyume cha sheria kwenye machimbo ulioachwa wakitafuta dhahabu zilizobaki , hili ni tatizo la kawaida Afrika Kusini. Zaidi ya wachimbaji haramu 1000 tayari wametoka katika wiki za karibuni huku polisi wakiwakamata na kulikuwa na maiti moja iliyopatikana. Haiko wazi kama wale waliobaki katika mgodi wa Stilfontein katika jimbo la NorthWest hawako tayari au hawakuweza kutoka nje ya shimo lenye urefu wa zaidi ya kilomita 2 chini ya ardhi. Ndugu na marafiki wakishinikiza kuwepo mabadiliko katika mfumo wa uchambaji madini ya dhahabu katika mgodi ambao wachimbaji haramu wamekwama, Afrika Kusini, Ijumaa, Nov 15, 2024. Ndugu na marafiki wakishinikiza kuwepo mabadiliko katika mfumo wa uchambaji madini ya dhahabu katika mgodi ambao wachimbaji haramu wamekwama, Afrika Kusini, Ijumaa, Nov 15, 2024. Polisi na wana jumuiya walisimama karibu na mlango wa mawe kwenye sehemu ya kuingilia ambako kulikuwa na kifaa kilichowekwa kwa ajili ya kuwavuta nje wanaume hao. Mwanafamilia Shona Roselina anasema: “ Ndio tunao wanafamilia zaidi ya 20 , waliokuja kutoka Chipinge nchini Zimbabwe. Tunatumai watatoka nje ili tuwapeleke nyumbani. Mmoja ana mke ambaye yuko hapa. Analia, hatujui jinsi ya kumsaidia. Mume wake alikwenda chini ya ardhi mwezi Aprili na amekuwa huko hadi sasa. Hakuna chakula , hakuna kitu. Tunajaribu kuwasaidia.” - Reuters #Stilfontein #madini #mgodi #dhahabu #wachimbaji #afrikakusini
wanafamilia wa wachimba madini haramu wakusanyika nje ya mgodi
- 22 Dec 2024 - Speaking at Kipkorgot AIC Church in Uasin Gishu on Sunday, the President stated that the project would eventually extend to Malaba, improving travel and trade along the corridor.
- 22 Dec 2024 - According to eyewitness reports, the driver of the speeding vehicle lost control at Mashinani area in Murumba, running over a bodaboda operator and his pillion passenger, both of whom were killed instantly.
- 22 Dec 2024 - The incident, reported at Narok Police Station, saw a 17-year-old girl arrested over the death of her 16-year-old kin.
- 22 Dec 2024 - The event stood out for its inclusivity and remarkable organization, with the majority of participants, including the best man, bridesmaids, and many attendees, also being members of the deaf community.
- 22 Dec 2024 - Here is what we know so far about the man who was arrested as the suspected driver in a car-ramming attack on Friday at a Christmas market in the German city of Magdeburg in which five people were killed and some 200 injured.
- 22 Dec 2024 - Speaking in Muhoroni, Ichung’wah emphasized the importance of cleansing the house spiritually and preventing such events from recurring.
- 22 Dec 2024 - A farmer has suffered a huge loss of more than Sh1milliion following the death of 198 goats killed by the wild animals suspected to be leopards.
- 22 Dec 2024 - Police in Homabay County on Friday arrested seven employees of a local restaurant in connection with the death of a fourth-year student from Tom Mboya University.
- 22 Dec 2024 - Occurs when breathing is partially obstructed while sleeping.
- 22 Dec 2024 - Homa Bay residents are set to begin benefitting from the long awaited multibillion development projects in the next three months.