Wanaharakati: Watu 1,700 watumiwa kufanya ushawishi COP29

  • | VOA Swahili
    544 views
    Kikundi cha wanaharakati walitumia nyoka mkubwa wa bandia kama nyenzo ya kufikisha ujumbe ndani ya ukumbi wa kongamano la COP 29 Ijumaa (Novemba 15) wakishinikiza kuwa watu wanaofanya ushawishi kwa niaba ya wachimbaji mafuta na gesi asilia katika mkutano huo kutolewa nje ambapo nchi mbalimbali zinajaribu kufikia makubaliano kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti ya Muungano wa kikundi cha Kick Out the Polluters Coalition ilisema zaidi ya washawishi 1,700 walikuwa wanahudhuria mkutano huo wa kila mwaka wa hali ya hewa. Mwaka 2023 kulikuwa na zaidi ya watu 2,400 waliokuwa wanafanya ushawishi kuhusu katika COP 28, lakini mahudhurio ya COP yalikuwa ni idadi kubwa zaidi kwa jumla. -Reuters #cop29 #azerbaijan #fossilfuels #voaafrica #lobbyists #maandamano #voa #voaswahili