Moto Uhispania wauwa watu 10 katika jumba la wastaafu

  • | VOA Swahili
    452 views
    Moto ulisababisha vifo vya takriban watu 10 katika jumba la wastaafu kaskazini mwa Uhispania, serikali ya mkoa wa Aragon imesema leo Ijumaa. Moto huo katika mji wa Villafranca del Ebro, kilomita 35 kusini mashariki mwa Zaragoza ulianza katika makazi ya wazee mapema leo. Ilichukua saa kadhaa kwa wafanyakazi wa zima moto kutoka eneo la Zaragoza kudhibiti moto huo, msemaji wa serikali ya mkoa alisema. Msemaji huyo hakusema iwapo waathirika wote walikuwa wakazi wa mji huo wa wastaafu, ambapo takriban watu 82 wanaishi hapo. Mtu mmoja alikuwa katika hali mbaya kiafya, huku watu kadhaa wengine wakipata huduma, haswa kutokana na kuvuta moshi. Chanzo cha moto huo bado kinaendelea kuchunguzwa. #moto #uhispania #vifo #makazi #wazee #wastaafu #jengo #aragon #zaragoza #voa #voaswahili