Mpito wa SHA waathiri huduma za afya

  • | KBC Video
    7 views

    Shirikisho la mawakili wa kike humu nchini, FIDA limeitaka wizara ya Afya kukumbatia mfumo wa haki za kimsingi katika utoaji huduma za afya. Chama hicho kimeonya kuwa mpito wa mfumo wa hazina ya kitaifa ya afya ya jamii SHIF, umefichua mapungufu makubwa ya kimfumo ambayo yameathiri upatikanaji wa huduma bora na za gharama nafuu za matibabu. Na kama anavyoripoti Timothy Kipnusu, chama hicho kinataka uhamisho huo kuendana na kanuni za utoaji huduma za afya kwa wote, kupunguza vikwazo vya kifedha, kuhakikisha uwepo wa rasilimali za kutosha na utunzi wa haki za walioathirika zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive