Magavana watishia kusitisha shughuli za serikali za kaunti

  • | KBC Video
    19 views

    Baraza la magavana limetoa onyo kali kwa wizara ya fedha likiitaka itoe mara moja pesa inazodaiwa na serikali za kaunti la sivyo lilemaze huduma za serikali za kaunti kote nchini katika muda wa siku 30 zijazo.Akiongea baada ya mkutano usiokuwa wa kawadia wa baraza hilo, mwenyekiti wake ambaye ni gavana wa wajir Ahmed Abdullahi alisema serikali za kaunti bado hazijapokea mgao wa kipindi cha sasa cha matumizi ya pesa za serikali .Kufikia sasa jumla ya shilingi billioni 63.6 bado hazijatolewa ambazo ni migao ya miezi ya Oktoba na Novemba pekee. lakini ikijibu madai hayo, wizara ya fedha imesema haidaiwi pesa zozote na serikali za kaunti ikisema pesa za mwisho ilizokuwa ikidaiwa ambazo ni shilingi billioni 30.8 zililipwa leo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive