Narc Kenya yajitoa Azimio

  • | Citizen TV
    1,156 views

    Chama cha Narc Kenya kinasema kimekamilisha mchakato wa kujiondoa kutoka muungano wa azimio la umoja one kenya. Kwenye mkutano na wajumbe wa chama hicho, kinara wa Narc Kenya Martha Karua amesema kuwa hatua ya kujiondoa kwenye muungano huo iliafikiwa baada ya vyama tanzu kwenye muungano huo kuonekana kuegemea upande wa serikali. Narc Kenya ilikuwa imetoa ilani kuhusu lengo lake kwa msajili wa vyama vya kisiasa.