Wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Standard Group wadai mabaki ya malipo

  • | Citizen TV
    460 views

    Wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Standard Group sasa wanaitaka kampuni hio kulipa mishahara yao iliyosalia haraka la sivyo wafanye maandamano. Wafanyakazi hao walioachishwa kazi mwaka huu na mwaka jana wamesema watafanya maandano jumanne ijayo endapo hawatalipwa. Wameikashifu kampuni hiyo kwa kuwapa ahadi za uongo, wakisema wamekuwa wakihangaika tangu walipoachishwa kazi.