Idadi ya waliofariki baada ya ukuta kuanguka Jomvu, Mombasa yafikia watu saba

  • | Citizen TV
    383 views

    Idadi ya waliofariki kutokana na mkasa wa ukuta kuanguka huko Miritini Mombasa imeongezeka hadi Saba. Mama mja mzito aliyekuwa na pacha amewapoteza watoto hao mapema hii leo huku familia zikifika katika hospitali ya Makadara kutaka kuchukua miili ya wapendwa wao. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki Gavana wa Mombasa amewaonya wanaoendelea na ujenzi wa mijengo duni kuwa chuma chao ki motoni.